Jun 6, 2012

Makundi ya kisiasa nchini Sudan yaunga mkono mazungumzo ya Khartoum na Juba



  Makundi ya kisiasa nchini Sudan yaunga mkono mazungumzo ya Khartoum na Juba Tume inayoundwa na vyama vya kisiasa nchini Sudan imetangaza kuyaunga mkono mazungumzo yaliyoanza katika mji mkuu wa wa Ethiopia Addis Ababa kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Taarifa zimeinukuu tume hiyo ilipokutana na ujumbe wa chama cha Congress ya kitaifa nchini humo na kuonyesha kuwa ina matarajio mazungumzo hayo yatafanikiwa.
Taarifa kutoka tume hiyo zinasema kuwa, mazungumzo ya mjini Addis Ababa yataziletea nchi mbili hizo, amani na utulivu. Naye katibu mkuu wa muungano wa vyama vya kisiasa nchini Sudan amewaambia waandishi wa habari kuwa, matatizo ya kiuchumi yatatatuliwa kwa kuwepo hali ya amani na utulivu wa ndani na nje ya nchi hiyo.
Tume za upatanishi kutoka Juba na Khartoum ziliwasili mji wa Addis Ababa Ethiopia wiki iliyopita, kwa lengo la kufanya mazungumzo ya kumaliza matatizo yaliyopo kati ya Sudan na Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment