Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame Makundi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo hii katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa huduma mpya ya tigo inayokwenda kwa jina la 'TIGO INTERNET MEGA BOKSI' ambapo alisema kuwa wateja wa tigo wataweza kujipatia vifurushi vipya vya mtandao vinavyo endana na mahitaji yao. Makundi alisema kuwa Mteja wa Tigo ataweza kununua kifurushi cha siku, wiki, au mwezi pamoja na kufanya uchaguzi unaoendana na matumizi mbali mbali ya huduma za kimtandao.alielezea namna ya kupata vifurushi hivyo kuwa ni, kwa kupiga *148*01# ambapo wateja watapata fursa ya kuchagua muda wa viofurushi wanavyovihitaji kulia ni Alice Maro afisa habari wa Tigo..
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakifuatilia uzinduzi wa huduma hiyo.
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame Makundi.
No comments:
Post a Comment