KAULI YA JAMES MBATIA KUHUSU MAUJI YA IRINGA.
                              Posted on 
                              Sep 6, 2012
                            |
                            
                                  No Comments
                                  

Wakati  bado kuna sintofahamu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha  Channel Ten, Daudi Mwangosi, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania  (TCD), James Mbatia (pichani), amewaonya Wanasiasa na Viongozi wa dini  kutotoa kauli nzito ambazo zinaweza kuhatarisha amani.
 Pia,  Mbatia pamoja na Viongozi wengine wa vyama vya siasa nchini vimemtaka  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kukaa kikao cha dharula ili kujadili suala  hilo kwa undani.
 Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mbatia alisema “Tunaungana  kulaani kwa nguvu zote, lakini hatutaki kuishia kulaani bali  tumejipanga sisi Wanasiasa kukutana na Waziri Mkuu pamoja na Msajili wa  vyama, Waziri Nchimbi na timu yake akiwemo IGP na mawaziri wengine  katika kikao cha dharula”
 Alienda  mbali zaidi na kusema Wanasiasa na Viongozi wa dini wametoa kauli nzito  nzito juu ya tukio husika lakini zinaweza kuipeka nchi pabaya.
 Badala yake alishauri nchi itulie katika kipindi hiki na Wanasiasa hao na Viongozi wa dini kuacha kutoa kauli hizo kwa sasa.
