WATOTO WA VIGOGO TANROADS WAFUKUZWA KWA KUGHUSHI
Posted on
Oct 25, 2012
|
No Comments
SERIKALI imewafukuza kazi watoto wa vigogo waliopata ajira bila ya
kufuata taratibu za kisheria katika mizani inayosimamiwa na Wakala wa
Ujenzi wa Barabara(Tanroads).
Hata hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kudai kuwa, kuna baadhi ya watoto wa vigogo wamepata ajira kinyume na taratibu.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuu (PAC), Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale alisema watoto hao waliajiriwa kimakosa.
Alisema watoto hao wametambuliwa na kwamba baadhi yao tayari wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi huku wengine vyeti vyao vikiendelea kukaguliwa.
“Kuna baadhi ya wafanyakazi walikuwa wamepata ajira kinyume na taratibu, hii inatokana na kupata ajira kwa kujuana lakini suala hili tayari tumelifanyia kazi na baadhi yao tumewafukuza,” alisema Mhandisi Mfugale.
Alisema kutokana na hali hiyo, wataendelea kuhakiki vyeti vya wafanyakazi wote na kuhakikisha kuwa, wanatangaza ajira upya ili wenye vigezo waweze kupitishwa na wasiokuwa navyo waondolewe.
Alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa, ajira zinazotolewa katika idara hiyo ni za muda mfupi, ili kuondoa mianya ya ajira za kujuana.
Aliwataka mameneja wote wa mikoa kufuata taratibu za kisheria katika kutoa ajira kwa wafanyakazi wapya.