RAIS ASSAD APEWA SAA 48 KUONDOKA NCHINI SYRIA.
Posted on
May 31, 2012
|
No Comments
Waasi wa Syria wamempa Rais Assad muda wa saa 48 wa kutekeleza mpango wa amani wa kimataifa ili kukomesha mauaji la siyvo ataona matokeo yake.
Katika tamko alilolitoa kwenye mtandao wa “You Tube”, Kanali Qassim Saadeddine amesema waasi watajitoa katika mapatano yote, hadi itakapofika leo adhuhuri na kuchukua hatua za kuwalinda raia na vijiji vyao.
Wakati huo huo Urusi na China zimeusisitiza msimamo wao wa kupinga kujiingiza kijeshi nchini Syria.
Hapo awali mjumbe wa kimataifa anaesuluhisha nchini Syria Bw. Kofi Annan amesema kuwa nchi hiyo sasa imefikia hatua ambapo hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
Wakati mapigano yanaendelea kati ya waasi na majeshi ya serikali, waangalizi wa kimataifa walizigundua maiti 13 mashariki mwa Syria.
Miili yao ilikuwa imefungwa na kuonyesha dalili kwamba waliuliwa kwa kupigwa risasi.

