ASHA ROSE MIGIRO AANGWA RASMI UN.
Posted on
Jun 30, 2012
|
No Comments
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe, Profesa Cleophas Migiro wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini.
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo amempogeza na kushukurusu sana Migiro kwa namna alivyokuwa mshauri wake na mwalimu wake ambaye a anasema kwa ualimu wake anampa alama ya plus plus plus. akatumia hafla hiyo kutangaza kwamba anamteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika. Migiro anaondoka baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka mitano na nusu.
Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa hafla hiyo, akatoa shukrani zake kwa Ban ki Moon kwa kumpatia heshima hiyo ya kihistoria ambayo haita kaa ifutike na kwamba ameupokea uteuzi huo kwa mikoni miwili na hasa kutokana na kwamba tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni tatizo ambalo analichukulia kwa uzito wa aina yake.
Hata kupiga picha naweza. Naibu Katibu Mkuu akinyaka tukio hili la picha wakati Katibu Mkuu Ban Ki Moon akizungumza na Bint wa mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.
