AWAMU YA TATU YA MGOMO WA MADAKTARI 23 JUNE 2012.
Posted on
Jun 19, 2012
|
No Comments
Baada ya kushuhudia migomo ya madaktari kwa awamu mbili na baadaye kufuatiwa na majadiliano yalioyoisha hivi karibuni sasa kuna kila dalili ya kutokea kwa mgomo mwingine mara itakapofika tarehe 23 juni 2012.
migomo miwili ya kwanza ilipuuzwa hivihivi lakini mwishowe tuliona viongozi wakuu wa nchi wakirudi nyuma na kuomba huruma ya mazungumnzo.
je iwapo mgomo wa tarehe tajwa utatokea ni nani alaumiwe kwa kushindwa kutatua mgogoro huu uliodumu kwa kipindi cha nusu mwaka sasa??
TAARIFA KWA UMMA MOROGORO.Katika kikao cha madaktari na wahudumu wa afya Ifakara kilichofanyika tarehe 16.June 2012, Kwa pamoja kilikataa taarifa iliyotolewa na serikali kuhusu madai ya Madaktari na Wahudumu wa Afya. Kikao kilitoa maazimio yafuatayo
1. Tunasikitishwa na msimamo wa serikali kutokuonyesha lengo la kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya.
2. Tunatangaza mgogoro rasmi dhidi ya serikali kuhusiana na madai yetu kudharauliwa na kutofanyiwa kazi.
3. Tutaungana na madaktari na wahudumu wengine wa afya Tanzania katika mgomo utakaoanza tarehe 23 Juni 2012. Kama Serikali haitafanyia kazi madai yetu
4. Tunaukumbusha umma kuwa serikali ilikuwa na muda wa kutosha kufanyia kazi na kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya
TAMKO BUGANDO:
Kutokana na kikao cha tarehe 15/06/2012 hapa Bugando na kanda ya Ziwa kwa ujumla tunatamka kwamba:-
1. Hatukubaliani na namna serikali ilivyo- na inavyoshughulikia suala la madaktari na wahudumu wengine wa afya hapa nchini.
2. Ni vema serikali itoe tamko lenye tija juu ya mgogoro unaondelea kati yake na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini
3. Tutaungana na madakrai wote pamoja na wahudumu wengine wa afya katika mgomo utakaonza tarehe 23/06/2012 ikiwa hatua madhubuti na zenye tija hazitachukuliwa
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki AfrikaTAMKO LA MADAKTARI NA WAHUDUMU WA AFYA DODOMA
Baada ya kupata muda wa kupitia na kuchambua kwa kina ufafanuzi wa serikali kuhusu madai ya madaktari. Madaktari na wahudumu wa afya Dodoma tunapenda kutoa tamko kama ifuatavyo
1. Tunaunga mkono maamuzi ya kikao cha madaktari na wahudumu wa afya cha tarehe 9/06/2012 kwa kuukataa ufafanuzi wa madai ya msingi kwani hauna nia ya dhati wa kuleta suluhisho la kudumu katika sekta ya afya. Hivyo tupo katika mgogoro na serikali na tutaungana na wenzetu katika mgomo utakaoanza tarehe 23/06/2012.
2. Tunaitaka serikali iache mara moja jitahada zake za kutugawa wahudumu wa sekta ya afya kwani kwa kufanya hivyo kutadhorotesha ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo tunaitaka serikali ianze mara moja kuwalipa wahudumu wote wa afya posho mpya za kuitwa kazini.3. Tunawaomba wahudumu wa afya wote na popote walipo kuendelea kuwa pamoja katika kutetea huduma bora na maslahi mazuri katika sekta ya afya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
