BALOZI WA JAMHURI YA DJIBOUTI-TANZANIA ASHEREHEKEA MIAKA 35 YA NCHI YAKE.
Posted on
Jun 26, 2012
|
No Comments
![]() |
Pichani juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akiongea machache kwenye hafla fupi ya kutimiza miaka 35,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo mabalozi kutoka sehemu mbalimbali,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo nyumbani kwa balozi huyo,jijini Dar.
![]() |
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akimpokea mgeni rasmi wa hafla hiyo,Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi alipokuwa akiwasili nyumbani kwa balozi huyo.
![]() |
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo akimkaribisha Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) mara alipokuwa akiwasili kwenye hafla hiyo.
![]() |
Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons) akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi jioni ya leo kwenye viunga vya balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo
![]() |
Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo akizungumza machache na machache na Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi ,shoto ni Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons)
![]() |
Balozi Shamo na Mkewe wakiwa na wageni wao waalikwa waliofika kujumuika nao kwenye hafla hiyo.
![]() |
Mke wa Balozi,Mariam Shamo (wa nne shoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
![]() |
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe Juhayna Kusaga wakifurahia jambo kwenye hafla hiyo
![]() |
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ally Hassan Mwinyi akizungumza jambo na Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons).










