photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > Bus lawaka Moto, abiria wanusurika..

Bus lawaka Moto, abiria wanusurika..

Posted on Jun 10, 2012 | No Comments


ABIRIA 65 waliokuwa wanasafiri kwa basi la Kampuni ya Moro Best, jana walinusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea kwa moto katika eno la Sanga Sanga mkoani Morogoro.
Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni zilisema kuwa, basi hilo lilikuwa likitoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kilombero, na kwamba chanzo ni hitilafu ya umeme na hivyo kuwaka moto na kuteketea lote pamoja na baadhi ya m izigo ya abiria.
Hata hivyo, chanzo chetu cha habari kilisema kuwa hakuna abiria yeyote aliyefariki wala kuumia katika ajali hiyo iliyotokea majira ya jioni na hivyo, harakati za kuwatafuta abiria usafiri mwingine zilikuwa zikiendelea.
Kuhusu hali ya usalama ni kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na abiria hao waliimarisha ulinzi wa mizigo, na hivyo hakuna upotevu wowote uliojitokeza kwa mali ziliokolewa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru