CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI ZA MITAA TANZANIA (TALGWU) KIMESIKITISHWA NA HATUA YA SERIKALI YA KUONGEZA MSHAHARA TSH. 170.000 BADALA YA 315.000
Posted on
Jun 26, 2012
|
No Comments
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimesikitishwa na hatua ya serikali ya kuongeza bajeti ya mishahara ya kima chini kwa mwaka 2012/2013, ambacho ni shl. 170,000 badala ya kilichopendekezwa awali sh.315,000.
Ongezeko la mshahara huo ni asilimia 20 kutoka kima cha chini cha Mshahara cha Shil.150,000 hadi kufikia sh.170,000 ongezeko ambalo ni dogo ukilinganisha na kupanda kwa gharama za maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Sudi Madega alidai kuwa kitendo cha serikali kuongeza kiwango hicho ni cha kikatili kwa sababu hakikidhi mahitaji ya wafanyakazi kwa ujumla.
Madega alichanganua kuwa, licha ya mishahara midogo wanayolipwa wafanyakazi hao katika sekta mbalimbali, lakini bado serikali imeshindwa kulipa madeni yao kwa wakati na kuwafanya waendelee kuishi maisha magumu.

