CHINA YAANDAA MAONYESHO YA KWANZA YA AINA YAKE YA BIDHAA BARANI AFRIKA YATAKAYOFANYIKA TANZANIA.
Posted on
Jun 26, 2012
|
No Comments
Mwakilishi Mkuu wa Kiuchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China hapa nchini Bw. Lin Zhi Yong akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusiana na kufanyika kwa maonyesho yatakayoitwa ‘Brands of China African Showcase 2012’. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu Msaidizi wa China Foreing Trade Guangzhou Exhibition Gereneal Corp. Bw. Ma Guo Qin na Bi. Yang Feng Lan. Wa kwanza kushoto ni Bw. Adam Zuku kutoka Tanzania Chamber of Commerce (TCCIA).
Bw. Adam Zuku kutoka Tanzania Chamber of Commerce (TCCIA) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na maonyesho hayo yatakayofanyika waka wa Sabasaba, na kusema kuwa China imefanya mchango chanya katika kutengeneza bidhaa zinazotimiza mahitaji ya watu wa Afrika, ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi kwa ujumla na jitihada za kuinua uchumi wa ndani na maendeleo ya jamii.
Katika kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa uchumi na biashara barani Afrika kati ya China na nchi za Afrika na kuonyesha bidhaa za Kichina katika soko la Afrika, serikali ya China imeandaa maonyesho yatakayojulikana kama ‘Brands of China African Showcase 2012’.
Maonyesho hayo yatakuwa ya kwanza ya aina hiyo kufanyika Afrika nzima, ambapo hafla hiyo imeandaliwa na na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano ya Watu wa China, Serikali za majimbo ya Jiangsu, Zhejiang na Guangdong na inatarajiwa kufanyika kuanzania Julai Mosi hado 5 2012 katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba.
Katika siku tano za maonyesho, kutafanyika kongamano kati ya kampuni hizo za kichina na wafanyabiashara wa Afrika ili kutoa nafasi ya ‘exhibitors’ na wanunuzi kuzungumza uso kwa uso na kubadilishana mawazo na mbinu za kibiashara.
