photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> IKULU:TASWIRA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA RAIS JAKAYA KIKWETE JIJINI ARUSHA

IKULU:TASWIRA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA RAIS JAKAYA KIKWETE JIJINI ARUSHA

Posted on Jun 1, 2012 | No Comments

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisamiana na Rais wa Japan International Cooperation Agency (JICA) Profesa Akihito Tanaka na baadaye kufanya naye mazungumzo   baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mshauri wa Mfalme wa Tano wa Morocco Bw Omar Kabbaj   baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Makhtar Diop baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana wa Arusha walioshiriki kutoa huduma kwa wajumbe wa  Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.Picha na IKULU

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru