KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KIKIWA KIMETELEKEZWA BARABARANI MOSHI
Posted on
Jun 28, 2012
|
No Comments
WIMBI la matukio ya wanawake kujifungua na kuwatelekeza watoto limekuwa likiongezeka nchini ambapo katika tukio la kusikitisha jeshi I la polisi mkoani Kilimanjaro, limemuokota kichanga kinacho dhaniwa kuwa ni cha siku moja kikiwa kimetelekezwa kando kando ya barabara ya kibosho , wilaya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro.
Akidhibitisha ukweli wa tukio hilo, kamanda mwandamizi wa jeshi la polisi la mkoani wa Kilimanjaro Robert Boaz , alisema, majira ya asubuhi ya jana, walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna kichanga kimettelekezwa katika barabara ya kibosho.
Kamanda Boaz, alisema kichanga hicho chenye jinsia ya kiume, kinakadiriwa kuwa ni cha siku moja, vijana wake walifika maeneo hayo na kumchukua na kumkimbiza katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa ajili ya uangalizi wa madaktari wakati uchunguzi wa tukio hilo likiendelea.
“Tulimkuta mtoto huyo katika hali nzuri tu na kwa usalama zaidi, tumempeleka katika hospitali ya KCMC, chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa watoto,” alisema Boaz na kuongeza kuwa
“ Askari wangu kwa sasa wanafanya uchunguzi ili kuweza kubaini ni nani aliyefanya kitendo hicho cha kinyama na tutakapofanikiwa kumkata hatua za kisheria zitachaukua mkondo wake,” alisema kamanda Boaz.
Kamanda boaz, alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo, kutoa taarifa ya mtu yeyote, aliyekuwa mjamzito awali na kwa sasa haupo kwa hali za kutatanisha, kutoa taarifa katika jeshi la polisi ili kuweza kumbaini mama wa mtoto huyo.
Na Mary Mosha,
Moshi.
