photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> Madaraka Day Kenya: Habida kutumbuiza Ikulu

Madaraka Day Kenya: Habida kutumbuiza Ikulu

Posted on Jun 1, 2012 | No Comments

Leo ikiwa ni siku ya Madaraka nchini Kenya mwanadada Habida amealikwa kutumbuiza Ikulu.

Kupitia Twitter, mrembo huyo amesema, “I'm a Dreamer is the song they asked me to sing today at state house listen to my unreleased track here http://www.habidasworld.com.”

Hata hivyo Habida amekuwa na wasiwasi na sauti yake kutokana na kusumbuliwa na homa, “Really hoping my voice holds up today, this homa is no joke!”

Kila June 1, wakenya duniani kote husherehekewa siku ya kuzaliwa upya kwa Kenya. Mwaka 1963 Kenya ilipewa uwezo wa kujitawala lakini Kenya iliupata uhuru wake rasmi December 12 mwaka huo huo.

Madaraka ni sikukuu ya kwanza ya kitaifa ambapo wakenya hukutana pamoja kusherehekea kwa kula, kunywa, kuimba na kucheza. Wengine hupanda miti kuadhimisha siku hii na kila mmoja huwakumbuka mashujaa walipigana na kufa kwa ajili ya uhuru wa nchi yao.

“I want to wish everyone a fantastic independence day! This is the anniversary of our rebirth, please remember what this day was about as u enjoy. Our ancestors who fought for our freedom hongera!” 
ameandika Habida.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru