Mali za Sh30 milioni zimeteketea Tanga
Posted on
Jun 9, 2012
|
No Comments
BIDHAA zenye thamani ya Sh30 millioni zimeteketea kwa moto uliotokea kwenye soko la Mgandini jijini Tanga juzi usiku.Akizungumza na waandishi habari, Katibu wa Ushirika wa Wafanyabiashara sokoni hapo, Riziwani Mwinyikheri alisema, wafanyabiashara wapatao 150 wameathirika na moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake hakijafahamika mara moja.
Ridhiwani alisema , moto huo umesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao na kwamba bidhaa mbalimbali zimeteketea kabisa.Alitaja bidhaa zilizoteketea kuwa ni pamoja na magunia ya mchele, unga, maharage na mbogamboga. Bidhaa nyingine ni ngano, mafuta na viazi.
Akielezea moto huo, Katibu huyo alisema, ulianza majira ya saa 9 alfajiri ambapo ulikolezwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma asubuhi na kusababisha kusambaa kwa haraka katika vibanda vingi sokoni hapo.Hata hivyo, Katibu huyo aliulalamikia Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kutowapa ushirikiano kwa kuwapatia gari la zima moto baada ya kuwapa taarifa ya moto huo.

“Nasikitika kueleza kuwa, tumewapa taarifa uongozi wa jiji la Tanga ya kuzuka moto sokoni hapa cha ajabu hawakuweza kutupa msaada wowote”,alisema Katibu huyo.
Hata hivyo, aliushukuru uongozi wa Mamlaka ya Bandari, Tanga kwa kuwapa ushirikiano na kuwapatia gari la zima moto pamoja na kuweza kuokoa baadhi ya mabanda yaliyosalia.
Baadhi ya waathirika walieleza wasiwasi wao kuhusiana na hali ya baadaye ya biashara zao hasa wakizingatia kuwa walichukua mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha.