Kwa wale mnaomfahamu mchungaji Gwajima mtakubaliana nami kuwa ni moja ya wachungaji wenye upako wa ajabu Tanzania na wanaozungumza mambo yaliyofunuliwa kwao na Mungu.

Katika mahubiri yake ya Jumapili na jana jioni alisema kwamba amefunuliwa kuwa Sitta na Mwakyembe kwakuwa ni watu waadilifu watashindwa ku-survive ndani ya CCM maana watakuwa wanachukiwa sana na kuwekewa mizengwe na hivyo watajiunga CHADEMA kabla ya uchaguzi mkuu 2015. Pia alitabiri CCM inakwenda kuanguka na utawala utakaojali maslahi ya nchi kuundwa.


Natamani mwaka 2015 ufike haraha ili tushuhudie unabii ukitimia! Ili ukubaliane na Mchungaji kuwa CCM inakwenda kuanguka, angalia kadi za CHADEMA zinavyotafutwa kama dhahabu mitaani. Kila mtu anaulizia kadi zinapatikana wapi, maji yamebadili mkondo, hakuna anayevutiwa tena na CCM