photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > NDOA NDOANO..

NDOA NDOANO..

Posted on Jun 5, 2012 | No Comments

Mke mlevi na mpenda starehe!

Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!


Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.
Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.
 
Ukitaka kushirikiana nasi habari yako tuma apa, rchugga@gmail.com

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru