photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > Rais Jakaya Kikwete azuiwa kusoma ripoti katika mkutano wa Umoja wa Afrika.

Rais Jakaya Kikwete azuiwa kusoma ripoti katika mkutano wa Umoja wa Afrika.

Posted on Jun 9, 2012 | No Comments

RAIS Jakaya Kikwete amezuiwa kuwasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa mpango wa Mpango wa kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM), kwa sababu ya madeni makubwa yanayotokana na kutowasilishwa kwa michango kwa ajili ya uendeshaji wa sekretarieti ya mpango huo.

Tanzania inadaiwa kiasi cha Dola za Marekani 800,000 sawa na Sh1.258 bilioni kwa kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha (exchange rate) vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambavyo ni wastani wa Sh1, 572.87 dhidi ya Dola ya Marekani.

Deni hilo ambalo ni malimbikizo ya ada ya Dola 100,000 kila mwaka kwa miaka minane mfululilizo tangu mwaka 2005 ni kashfa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inayoongozwa na Waziri Benard Membe, ambayo mpango wa APRM unatekelezwa chini yake.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru