Rais wa Malawi, Joyce Banda, ameamua kuuza ndege ya rais pamoja na magari 60 ya fakhari.
Posted on
Jun 3, 2012
|
No Comments
Ndege hiyo ilinunuliwa kwa dola milioni-13 na rais aliyemtangulia, Bingu wa Mutharika, aliyefariki mwezi wa Aprili.
Rais Banda amenukuliwa kusema kwamba anatosheka kusafiri kwenye ndege za abiria kama watu wengine, kwa sababu ameshazowea kutembea kwa miguu na kusaidiwa na wasafiri njiani.
Fedha zitazopatikana katika mauzo ya ndege na magari hayo, zitatumiwa kuwasaidia maskini wa Malawi.
Serikali ya Uingereza, ambayo ndio mfadhili mkubwa wa koloni lake hilo la zamani, imepokea vema uamuzi huo kuwa ni ishara inayotia moyo.
Swali ni kwamba Tanzania imejifunza nini kutokana na hili!!!.
