photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > RC Arusha awamkali kwa wakandarasi wa Barabara za Arusha..

RC Arusha awamkali kwa wakandarasi wa Barabara za Arusha..

Posted on Jun 6, 2012 | No Comments


Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia wakandarasi wa barabara ambao hawajui kazi zao na hawana vigezo kuendelea kutengeneza barabara za mjini hapa kwani wanaweza kuwaletea madhara hapo baadae.
Hayo  juzi lipokuwa akifanya ziara yake ya ukaguzi wa barabara mbalimbali zinazojengwa  katika kati ya jijini hapa ambapo barabara nyingi zimeonekana kuchibwa na kuachwa  na mashimo bila ya kufanyiwa kazi hali inayosababishia jiji la Arusha kuwa na msongamano mkubwa wa magari.
Alibainisha wakandarasi ambao wamepewa kufanya kazi hiyo wamekuwa wanashindwa kufanya kazi ya ujenzi wa barabara kwa wakati kwani tangu wamepewa kazi hiyo wameshindwa kuonyesha kazi waliyofanya kwa kipindi kizima cha miezi saba ambayo wameanza na ndo imemalizika katika  kazi hiyo ,na hamna kitu walichofanya wakati mradi huo unatakiwa ukabidhiwe Januari 31 mwakani 2013 kwani ni mradi wa miezi 15.
mulugo alibainisha kuwa iwapo makandarasi huyo ataendelea kufanya vitu hivyo basi  wao kama mkoa watafanya apili wao kama serekali na watatuma taarifa kwa benki ya dunia ambayo ndio imetoa fedha hizo za ujenzi wabarabara za jijini hapa kuwa mkandarasi huyo awafai katika kazi kwani anafanya kazi pasipo mipangilio nakujali muda.
"sasa leo tunakuja site na hawa wakandarasi wanajua kabisa twaja miezi saba imeisha hatujaona kitu kinachotengenezwa zaidi ya haya mashimo waliyoyachimba ambayo yanaababishia wananchi wetu kero kubwa kwani hawaoni sehemu za kupita kwa ajili ya mashimo wanasabishia mji wetu kuwa na msongamano wa magari kwa ajili ya wao wanafanya vitu kama hawataki vile sasa nasema sisi tutaapili kama hawatajirekebisha"alisema mulugo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru