Sakata la Mikopo kwa watanzania wanaosoma nchini Algeria.
Posted on
Jun 7, 2012
|
No Comments
Lile sakata la mkopo kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko mjini Constantine nchini Algeria linaendelea kuchukua sura mpya huku mambo yakiwa kitendawili ni lini fedha hizo zitatumwa kwa wanafunzi hao.
Habari kutoka chanzo chetu kilichopo huko nchini Algeria zinasema kuwa wanafunzi hao waliamua kuunda kamati yao ya kushughulikia jambo hili baada ya kuona wanazungushwa na kupigwa kalenda na umoja wa wanafunzi uliopo huko uitwao ATSA. Kamati hiyo ilipewa majukumu ya kupiga simu kwa mkurugenzi mtendaji wa bodi ambaye hakupokea simu hata moja kati ya zile zaidi ya 5 zilizopigwa.
Wakati taarifa zilizopo sasa ni kwamba bodi ya mikopo ilipokea akaunti hizo mnamo tarehe 25/5/2012 lakini kabla ya hapo vijana hao walishatumiwa e-mail na uongozi huo wakitaarifiwa juu ya akaunti zao kupokelewa bodi ya mkopo.E-mail hiyo ambayo pia ilitumwa kwa wanafunzi wote walioko nchini huko. Chanzo chetu kilitufowadia e-mail hiyo na tukakopi baadhi ya maandishi ya e-mail hiyo ambayo inasadikiwa kutumwa na waziri mkuu wa chama hiko ambaye tusingependa kumtaja jina :

