SOMA HABARI YA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR.
Posted on
Jun 28, 2012
|
No Comments
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Ferej, akiwasilisha hutuba ya Bajeti ya Ofisi yake katka Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi jana jioni katika ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako tukufu sasa likae kama Kamati ya matumizi ili liweze kupokea, kuzingatia, kujadili, kuchangia na hatimae liweze kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa mwaka wa Fedha 2012/2013.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana leo hii katika Baraza hili tukufu, kwa lengo la kujadili masuala muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
3. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya viongozi na wafanyakazi wote wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, napenda kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya kazi ya kuwahudumia wananchi. Utaratibu aliouanzisha wa kukutana na taasisi za Serikali na kupokea taarifa za utekelezaji wa kila robo mwaka una madhumuni ya kukuza ufanisi katika utendaji wa shughuli za Serikali ili kuweza kuwatumikia wananchi vizuri zaidi.Kusoma Nzima Ya Bajeti Ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
