photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Huyu apa...

Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Huyu apa...

Posted on Jun 5, 2012 | No Comments

Spika wa tatu wa Bunge jipya la Afrika Mashariki (EALA) Margaret Banbtonbg
Zziwa (49) kutoka Uganda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo uliopo
katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo. Zziwa ambaye ni Mchumi kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote*.(Picha na Mroki Mroki)
 
WABUNGE wa bunge la Afrika mashariki wamemchagua spika wa bunge hilo  kutoka nchini Uganda ambaye ataliongoza bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Spika huyo ambaye ndio mwanamke wa kwanza  kushika wadhifa huo wa juu katika bunge hilo ni  Magreth Zziwa kutoka nchini Uganda mbaye alimbwaga mpizani wake  Dora  Byamukama kwa kupata kura 33   Dora pia anatoka  nchini Uganda yeye alipata kura 12.

Awali matokeo ya kura hayakumpa Zziwa nafasi hiyo baada ya kupata kura 27  huku mpinzani  wake kura 18 na kufanya uchaguzi huo kurudiwa upya.
Aidha Mwanamama huyo ataliongoza bunge hilo kuanzia sasa  ni msomi mchumi mwenye shahada ya uzamili wa sayansi ya siasa na uchumi.

Mara baada kuchaguliwa Spika huyo aliapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge hilo ambapo baada ya kula kiapo aliwashukuru wabunge wa bunge hilo kwa kumchagua.

“Naishukuru serikali yangu ya Uganda na pia wananchi wa Uganda na ninyi wabunge kwa kunichagua kushika wadhifa huu nawaomba ushirikiano tuendleze jumuiya yetu”alisema Zziwa.

Mara baada ya zoezi hilo wabunge 45 wa jumuiya waliapishwa rasmi kuwa wabunge wa bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uchaguzi huo wa spika wa bunge hilo ulihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za afraka mashariki na baadhi ya ndugu waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo kwa  njia ya luninga zilizofungwa nje ya ukumbi wa bunge hilo walipongeza namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Bunge hilo ambalo linazinduliwa kwa mara ya  tatu na kuongozwa na Maspika kutoka nchi wanachama ambao huchaguliwa kwa kupokezana lilianza mwaka 2001 ambapo liliongozwa na Spika kutoka Tanzani Abdulrahaman Kinana kabla ya kupokelewa na Mkenya anayemaliza muda wake Abdrahin Abdi.

Kazi kubwa ya bunge la Afrika Mashariki ni kusimamia na kutunga sheria mbalimbali  za uendeshaji wa mambo katika jumuiya hiyo iliyo mbioni kuwa shirikisho la Afrika mashariki

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru