photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> TTCL WATANGAZA KUMNASA MHUJUMU MKONGO.

TTCL WATANGAZA KUMNASA MHUJUMU MKONGO.

Posted on Jun 27, 2012 | No Comments

SHIRIKA la Simu Tanzania (TTCL)  kwa kukishirikiana na polisi mkoani Mtwara wamemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za kuiba nyaya za mkongo.Anadaiwa kukutwa na nyaya ya urefu wa mita 100 uliokuwa ukitoa huduma ya  “data-voice” kwa wateja wao.Kufuatia wizi huo TTCL imepata  hasara ya Sh5 milioni na kuwakosesha huduma wateja wasiopungua 60.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Mtwara,  Abdul Mandrai alisema mtuhumiwa alikamatwa katika upekuzi  ambapo walikuta pia  mzani aliokuwa akiutumia kupima uzito wa mkongo huo.Mandrai alisema mkongo huo ukichomwa nyanya zake ni madini ya copper, ambapo alikuwa anauza kama vyuma chakavu bila kujua thamani yake.
Alisema mazingira aliyokutwa nayo mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa maeneo ya Chipuputa Mkanaredi yalionyesha kuwa ni mwizi mzoefu kwa kuwa sehemu ambayo huchomea mkongo huo  imeonyesha kuwa na usugu wa majivu.
Meneja huyo alisema kuwa katika eneo hilo kumekuwa na matukio ya mara kwa mara kutokea hivyo kusababisha shirika kuingia gharama za kuweka walinzi ambao wamefanikisha kumkama  mwizi huyo.
“ Tunawaomba wananchi watupe ushirikiano wa hali ya juu kwa kuwa unapotoa taarifa na kufanikisha kukamatwa mwizi unalipwa  Sh300,000” alisema Mandrai
Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu Mkoa wa Mtwara, Bakari Kilango alisema kuwa wananchi washirikiane kufichua wahalifu.

Polisi Mkoa wa Mtwara walithibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anatarajiwa kufikisha mahakamani.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru