photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> UN yateta kuhusu umuhimu wa mazingira katika siku ya mazingira dunia..

UN yateta kuhusu umuhimu wa mazingira katika siku ya mazingira dunia..

Posted on Jun 5, 2012 | No Comments

Mratibu  wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye lengo la  kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22 nchini  Brazil kwa niaba  ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise  Chamberlain. Kulia ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale inapotaka kwenda. Katikati  ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema Tanzania imeandaa  Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini walioshiriki warsha iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mtaifa kuhusiana na Umuhimu wa kufahamu na kutunza mazingira ikiwa ni katika Siku ya kuadhimisha Mazingira Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru