Wafanyabiashara ndogondogo wazidi kunyimwa raha na mgambo wa jiji..
Posted on
Jun 12, 2012
|
No Comments
Mgambo wa jiji wakiwa wamemkamata muuza machungwa mtaa wa Makunganya jijini Dar leo jioni.
...Songa mbele kijana.
Mgambo wa jiji wamekuwa na tabia ya kuwasumbua wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar hali ambayo inasababisha watu hao kushindwa kutafuta riziki yao ya kila siku. Mwandishi wa habari hii alipozungumza na baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hili, walionekana kusikitishwa na kitendo cha mgambo hawa kuwanyanyasa wafanyabiashara hao.
