WALIMU WANNE WAPANDISHWA MAHAKAMANI MKOANI ARUSHA.
Posted on
Jun 22, 2012
|
No Comments
Walimu wanne akiwemo mkuu wa shule ya Sekondari ya Moshono Jijini Arusha wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuiba fedha za shule na kusababisha hasara kubwa sana
Wakisomewa mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Ngwanta Mwakunga na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Rehema Mteta washitakiwa hao walifanya makosa hayo kwa nyakati tofauti tofauti
Aidha ilisemekana kuwa Mshitakiwa wa kwanza ambaye alikuwa ni mtumishi wa Serikali kati ya mwezi January na September aliiba kiasi cha shilingi milioni 4.8 kutoka katika shule ya sekondari ya Moshono.
Mshitakiwa wa pili ambaye ni Dismas Lewigo naye aliiba kiasi cha shilingi milioni 4 laki 6 ambapo ilikuwa ni kati ya June 2009 na 2010 hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana kwa Serikali
Mshitakiwa wa Tatu ambaye ni Lea Mwakenda aliiba kiasi cha shilingi Milioni 2 laki 3 wakati mshitakiwa wa Nne Zinyangwa Mcharo naye aliiba kiasi cha zaidi ya Milioni 11
Kesi hiyo itatajwa tena July 19 washitakiwa waliachiwa huru kwa dhamana ya shilingi Milioni 5 wakati kwa mshitakiwa wa mwisho ni kiasi cha shilingi million 4 pamoja na mali isiyoamishika.
