photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > Wamiliki wa maduka ya madawa watadharishwa mkoani Arusha.

Wamiliki wa maduka ya madawa watadharishwa mkoani Arusha.

Posted on Jun 11, 2012 | No Comments

WAMILIKI wa Maduka ya dawa baridi, wametahadhrishwa kutokuchukua dawa katika hospital za serikali na kuzipeleka kwenye maduka yao  kwa ajili ya biashara huku hospital zikiwa hazina dawa kwa ajili ya wagonjwa.

Hayo yameelezwa jana na mganga mkuu wa mkoa wa Arusha, Dk. Frida Mokiti, alipokuwa akifungua mafunzo ya wiki moja ya watoa dawa  katika maduka ya dawa muhimu, inayoshirikisha wauzaji wa dawa kutoka halamashauri ya Jiji la Arusha na wilaya ya Arusha DC,katika ukumbi wa chuo cha Ufundi, Arusha yaliyoandaliwa na mamlaka ya Chakula na dawa..

Dakta, Mokiti, alisema  kuwa kuna baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa ambao wamekuwa wakitumia ujanja kujipatia dawa hizo kutoka katika hosipital za serikalini na kuzipeleka kwenye maduka yao huku wagonjwa wakibakia bila dawa hivyo akawaonya kuacha tabia hiyo mara moja kwani msako utapita na atakaepatikana akiuza dawa hizo atakabiliwa na wakati mgumu.

Alisema lengo la serikali kutoa  mafunzo hayo kwa watoa dawa katika maduka ya dawa muhimu, ni ili kuwawezesha kupata elimu bora ya utoaji sahihi wa dawa na hivyo kuweza kuondoa tatizo huduma hafifu mkoani Arusha.

Alisema mafunzo hayo ambayo yanalenga katika sheria na kanuni zinazosimamia dawa sanjari na magonjwa yatokeayo mara kwa mara ,matibabu ya magonjwa  ya watoto kwa uwiano ,elimu ya ukimwi  na ushauri nasaha ,mbinu mbalimbali za mawasiliano  na elimu ya uzazi wa mpango.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru