Waziri mwingine ajiuzulu nchini Kuwait kufuatia shinikizo.
Posted on
Jun 12, 2012
|
No Comments
Waziri wa masuala ya jamii na kazi nchini Kuwait Ahmed al-Rujaib (Pichani) amejiuzulu wadhfa wake akiwa ni waziri wa pili kujiuzulu katika muda wa wiki chache baada ya kushinikizwa na wabunge wa upinzani.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaamini hatua hiyo huenda ikasababisha mabadiliko kamili ya baraza la mawaziri au kujiuzulu kabisa kwa serikali ya sasa ilioundwa baada ya uchaguzi wa mapema mwezi februari, hiyo ikiwa ni serikali ya nne katika muda wa miaka sita.
Wabunge wa kambi ya upinzani wamekuwa wakitaka waziri al-Rujaib ajibu maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu, udhibiti wa ubora wa chakula, vibali vya ukaazi na makampuni haramu.

