AISHA BAKARI MISS MARA 2012.
Posted on
Jul 2, 2012
|
No Comments
Redds Miss Mara 2012, Aisha Bakari (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili Eugenia Fabiano (kushoto) na mrembo aliyeshika nafasi ya tatu Jacqueline Mzava. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki Musoma Club.

Tano bora hiyo hapo.Upande wa Zawadi Mshindi wa Kwanza alipata sh 600,000/=, Mshindi wa Pili alipata Sh 400,000/=, Mshindi wa Tatu alipata 200,000/= , Mshindi wa Nne na wa Tano walipata 100,000/= na waliobaki walipata sh 60,000/= kila mmoja.
Mashindano ya Urembo Redd's Miss Mara 2012 yamefanyika kwa ufanisi Mkubwa katika ukumbi wa Musoma Club Mjini Musoma.Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini Mh Jackson Msome. Wageni waalikwa ni Lisa Jensen (Miss World Tanzania) ambaye amewahi kuwa Miss Mara 2006 na Miss Tanzania no 3. Pia alikuwepo Irene Karugaba Miss Mwanza na Mshiriki wa Miss Tanzania aliyepata nafasi ya kuingia (Top 10).
Majaji wa shindano wakiwa kazini
Shindano hili lilidhaminiwa kwa Kiwango kikubwa na African Barrick Gold Mine Ltd pamoja Tbl ambao ni Wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, Wadhamini wengine ni Musoma Club, Hotel Maltivilla, Mara Security Guard, Musoma Utalii Collage, Msendo Min Supermarket na Crdb.

