BRADLEY WIGGINS! MUINGEREZA WA KWANZA KUSHINDA TOUR DE FRANCE 2012.
Posted on
Jul 23, 2012
|
No Comments

Bradley Wiggins amekuwa Muingereza wa kwanza kushinda mashindano ya baiskeli ya Tour de France huku Mark Cavendish akifanikiwa kutawala hatua za mbio hizo kwa siku nne mfululizo.
Wiggins mwenye umri wa miaka 32 alimalizia mashindano hayo katika mitaa ya jiji la Paris kwa ushindi mwembamba wa dakika tatu na sekunde ishirini na moja.
Mwanatimu mwenzake kutoka timu ya Team Sky, ya Uingereza Chris Froome alishikilia nafasi ya pili na Vincenzo Nibali wa Italy nafasi ya tatu.
Cavendish alitawala hatua ishirini na tatu za mashindano hayo.