IFM YATIMIZA MIAKA 40 TANGU KUANZISHWA MWAKA 1972
Posted on
Jul 6, 2012
|
No Comments
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja akifungua pazia (leo) jijini Dar es salaam kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilipoanzishwa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika banda la Wizara ya Fedha kwenya maonyesho ya 36 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja amesema kuwa Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ili kiendelea kuzalisha wataalam mbalimbali watakaochangia kuleta maendeleo nchini.
Alisema kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwa muhimu katika kuwaendeleza vijana na hata watumishi waliopo kazini na hivyo kuboresha kada mbalimbali ikiwemo elimu juu ya masuala ya bima na fedha.
Hivyo ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika Chuo hicho kwa ajili ya kupata utalaam ambazo utawasaidia wao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Khijja alisema katika ya sasa ni vema wazazi wakawapatia watoto wao elimu kwani ndio itakayowakomboa.
