photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> KUTOKA VYUONI..

KUTOKA VYUONI..

Posted on Jul 6, 2012 | No Comments

CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA CHA ANZA KUTUMIA FURSA ZA EAC, CHA SAINI MAKUBALIANO NA CHUO KIKUU MAKERERE UGANDA NA CHUO CHA KIKUU CHA KIKRISTO.


CHUO kikuu  cha Tumaini Makumira  kimeingia katika makubaliano  ya ushirikiano  wa masuala  ya  kitaaluma na utafiti na vyuo  vikuu viwili  vya Makerere na  chuo kikuu cha Kikristo vyote  vya  nchini Uganda .
Hatua hiyo imeelezwa na pande zote kuwa ni kuonyesha kwa vitendo nia ya kutumia fursa  za kitaaluma zilizopo katika nchi wanachama  wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Makumira  Mchungaji Profesa Parsalaw ,akizungumzia hatua hiyo alisema kuwa  vyuo hivyo vitabadilishana pia machapisho mbalimbali ya kitaaluma katika nyanja za utawala na viwango bora vya kitaaluma.
Profesa Parsalaw alifafanua kuwa makubaliano ya Chuo Kikuu Makere yalisainiwa baina yake na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Makerere  Venancius Baryamureeba kwa niaba ya Chuo Kikuu Makere   na kuwa mkataba huo ulisaini wa katika mji  wa Kampala .
Aliendelea kubainisha kuwa mkataba mwingine ulisainiwa kati ya Profesa huyo kwa niaba ya Chuo Kikuu Tumaini na Mchungaji Daktari Senyonyi wa Chuo cha Kikristo(Uganda Christian University(UCU) ambapo sherehe fupi za kusaini makubaliano hayo, yalifanyika Mkono  Uganda.
Mchungaji huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa maeneo wanayotarajia kushirikiana ni eneo la Utafiti ,Ushauri ,Machapisho ya kitaaluma ,Sayansi na Teknolojia ,Kilimo na Mazingira,Sayansi jamii na Elimu ya Sheria ,kubadillishana wataalam ikiwa ni pamoja na wahadhiri wa vyuo hivyo .
Nyingine ni kuwapatia fursa Wanafunzi wa Vyuo hivyo kwenda kusoma na kubadilisha uzoefu pamoja na kubadilisha mitala ya taaluma
Kwa upande wake Profesa Venancius Baryamureeba  wa Chuo Kikuu Makerere Uganda akizungumzia makubaliano hayo alisema kuwa Ushirikiano huo utafungua milango kwa Wanafunzi katika vyuo hivyo kutembeleana na kujifunza ,hatimaye kuboresha taaluma zao na kujiamini .
Baryamureeba alibainisha kuwa Tanzania na Uganda ni kitu kimoja kwa kuzingatia ukweli kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ,ambayo imeundwa kwa pamoja kuboresha maslahi ya wananchi wa nchi mwanachama ,ikiwa ni kushirikiana katika soko la pamoja.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru