photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> NAPE: MZEE SABODO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.

NAPE: MZEE SABODO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.

Posted on Jul 6, 2012 | No Comments

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicheka bila uhasama na viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.
Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.
       Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.
       Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote haya yamefanywa na serikali ya CCM.
       Sasa kama serikali ya CCM imefanya hivyo, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya hivyo ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!
      Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!
     Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru