photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
  • Home
  • Buy / Sell
  • Jobs
  • Entertainment
  • Contact Us
> NDOANDOANO > NDOA NDOANO; HAWA NDIO WANAUME WANAONGOZA KUVUNJA NDOA ZA WATU
  • « Nyuma
  • | Mbele »

NDOA NDOANO; HAWA NDIO WANAUME WANAONGOZA KUVUNJA NDOA ZA WATU

Posted on Jul 23, 2012 | 1 Comment

NDUGU zangu, katika maisha ya sasa kuna watu flani ambao ukiona wana ukaribu uliopitiliza kwa mke wako, jua kuna jambo nyuma ya pazia na ukishangaashangaa unaweza kujikuta unamegewa penzi lako hivihivi.
Hiki nitakachokielezea leo nimekifanyia uchunguzi wa muda mrefu na kwa wale waliokumbana na hali halisi ya mambo, watakubaliana nami kwa asilimia zote. Juzi nilipata bahati ya kusuluhisha ugomvi wa rafiki yangu ambaye yeye na mkewe ni wafanyabiashara.
Chanzo cha ugomvi wao ni daktari mmoja ambaye inaonekana kwa muda mrefu amekuwa ‘akiitafuna’ ndoa yao na siku hiyo ndiyo ule msemo wa za mwizi arobaini ulipotimia. Rafiki yangu huyo alinasa sms kutoka kwa dokta huyo akitaka wakutane na mkewe siku hiyo.
Bahati ni kwamba, mwanaume huyo alikuwa akimpenda sana mke wake na hata nilipomshauri amsamehe waanze ukurasa mpya, alinielewa.
Lakini wakati hilo likitokea, jana yake nilisoma habari ya mke wa mtu aliyefumaniwa na kijana mmoja ambaye ni muuza genge mtaani kwao. Aibu ilioje kwa mwanamke huyo! Hivi inakuwaje mpaka mke wa mtu ambaye mume wake anahangaika juani kutafuta noti kisha mkewe huku nyuma anatoa penzi kwa muuza genge kirahisi? Hii inauma sana!
Matukio hayo mawili yalinifanya nifikie hatua ya kuandika makala haya juu ya watu wanaongoza kwa kusambaratisha ndoa za watu.
Muuza genge
Kuna tabia ambayo baadhi ya wanawake walio katika ndoa wanayo ya kubana matumizi yao ya kila siku kwa lengo la kuweka fedha za kufanyia mambo mengine baadaye.
Katika mazingira hayo wapo wanaojiweka karibu sana na watu hao wakiamini watapewa vitu vya bure kama vile nyanya, vitunguu nk. Wanawake wa sampuli hii wakikutana na wauza genge viwembe hawawezi kupona na ndiyo maana mwanaume anashauriwa kuwa makini sana na wauza magenge.

Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.


Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.

Muuza duka
Mama mmoja ambaye mume wake anafanya biashara za kusafiri mikoani alinaswa na mpangaji ambaye kwenye nyumba anayoishi mwanaume huyo ana duka. Baada ya tukio hilo ilibainika mama huyo alikuwa na tabia ya kuchukua vitu dukani hapo na siku hiyo alipotakiwa kulipa alimwambia kimasihara kuwa, yeye hana fedha kama vipi wamalizane kwa njia nyingine.
Kama mwanamke huyu alivyosema, wapo wake za watu ambao wamekuwa wakijirahisi sana kwa wauza duka wakijua itakuwa rahisi kwao kuambulia vitu vidogodogo na fedha. Kwa maana hiyo mkeo si wa kumruhusu kuwa na uhusiano wa karibu sana na wauza duka.

Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.


Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook
Habari Zilizo Mpya »
« Habari Zilizopita

Comments:1

  1. AnonymousJuly 24, 2012 at 1:26 AM

    Hata Wanawake sio waaminifu siku hizi,kwani lazima amkubali mwanaume anayemtongoza ilhali anajijua ye ni mke wa mtu?Msimamo muhimu haijalishi mumeo ana kipato gani!

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
Add comment
Load more...

Recent Hits

Charls Sons Construction Ltd.

Charls Sons Construction Ltd.

French Collections

French Collections

This could be your advert.

Photobucket

Total Pageviews

Chart / Comments

Popular Posts

  • TANZANIA TO CREATE CITY AROUND KILIMANJARO
    Tanzania plans to construct a city around its Kilimanjaro International Airport (KIA) to tap into tourism and business opportunities. The...
  • NAFASI ZA KAZI 20 BANK OF TANZANIA (BOT)
    Messenger (6 Posts) BOT Date Listed: Jul 10, 2012 Phone: No Calls Please Area: D...
  • MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI HIZI HAPA..!
    Mwili wa mwanamke ni tofauti na wa mwanaume linapokuja swala la kujamiiana. Mwanaume ni rahisi sana kupata ashki hasa akiona mwili wa mwa...
  • MATOKEA YA FORM FOUR MWAKA 2012 HAYA HAPA>>
    NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA CSEE 2012 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES Tafadhali jaribu kwa kubofya  hapa  au  hapa Tovuti ya ...
  • WATU 34 WAFARIKI KIWANDANI NCHINI INDIA
    Kiwanda cha fataki nchini India Watu 34 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa...
  • NAFASI ZA KAZI. USA EMBASSY
    Administrative Assistant USA Embassy Date Listed: Sep 3, 2012 Phone: No Calls Please ...
  • THESE ARE THE OWNERS OF JAMII FORUM
    Six years ago, a young man and a teenager sat down and planned to create an online user-generated news platform. Then it looked like...
  • WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKANUSHA UVUMI JUU YA KUHAMISHWA KWA WAMASAI SERENGETI
    Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki amekanusha uvumi unaosambazwa na Shirika moja kupitia mtandao wa...
  • PICHA NA HABARI KAMILI ZA MLIPUKO WA BOM ARUSHA.
    Watanzania wenzangu, Kwanza niwape pole kwa yaliyotokea Arusha asubuhi hii, hili ni tukio la kusikitisha na linalosta...

Categories

  • BURUDANI ( 16 )
  • BUSINESS ( 3 )
  • Buy / Sell ( 44 )
  • CHEKECHA ( 129 )
  • Dj.ManGi1 ( 74 )
  • Entertainment ( 205 )
  • Experience Tanzania ( 64 )
  • FRENCH COLLECTION ( 92 )
  • HOT LOOKS ( 14 )
  • INTERNATIONAL NEWS ( 295 )
  • INTERNATIONAL NEWS ( 2 )
  • Jobs ( 145 )
  • KIBONZO CHA SIKU ( 185 )
  • KUTOKA VYUONI ( 19 )
  • LIVE ON TV. ( 55 )
  • LOCAL NEWS ( 865 )
  • MAKALA ( 94 )
  • NDOANDOANO ( 171 )
  • PICTURE OF THE WEEK ( 23 )
  • POLITICS ( 129 )
  • SPORTS ( 255 )
  • TECHNOLOGY ( 1 )
  • UNAKUMBUKA ( 25 )
  • WAMETOKELEZEA ( 42 )
TOP

Copyright 2012 © RChugga Blog. All Rights Reserved. | Modified by MKCT