photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > STEVE NYERERE KUMKABIDHI MAMA NYERERE ZAWADI YA MOVIE.

STEVE NYERERE KUMKABIDHI MAMA NYERERE ZAWADI YA MOVIE.

Posted on Jul 5, 2012 | No Comments

Steven Nyerere akisalimiana na mama Nyerere
Jb akisalimiana na mama Nyerere

Mwigizaji wa filamu nchini Steve Mangele ‘Steve Nyerere amekabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa mke wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake,baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.
Steve alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi

Amesema, Mama Maria Nyerere alimsaidia sana kujifunza mengi kumhusu baba wetu wa taifa ikiwemo kumuonyesha vitu gani Mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda,na hata na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambao walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru