photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > AUWSA YAPANDISHA BEI YA MAJI ARUSHA.

AUWSA YAPANDISHA BEI YA MAJI ARUSHA.

Posted on Aug 30, 2012 | No Comments

Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Juliana
Na Mwandishi wetu;  Bilhuda Msangi
 Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mkoani Arusha AUWSA inatarajia kupandisha gharama za maji kutoka wastani wa shilingi 495 kwa mita moja ya ujazo na kuwa shilingi 1,175.66 kwa sasa na baadaye kuwa shilingi 1,307.54 kuanzia Julai mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa uchumi Ewura filex Ngamlagosi kwa niaba ya bodi ya mamlaka ya majisafi na majitaka  katika mkutano uliowashirikisha wananchi kutoa maoni yao kuhusu ongezeko la kupanda kwa huduma za maji uliofanyika mjini Arusha.

Mwakilishi Ewura Mayrose Kavura Majinge
Amesema  sababu ya kupandisha bei ya maji ni kutokana na mfumuko wa bei,kuongezeka kwa gharama za uendeshaji ikijumuisha gharama za umeme,ununuzi wa dira za maji na mafuta pamoja na kuendeleza miradi ambayo gharama zake ni zaidi ya bilioni 11.
Ameongeza kuwa faida ya ongezeko la bei ya majisafi na gharama za uondoaji majitaka litawezesha mamlaka kuongeza vyanzo vya  maji,kupanua huduma zake kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na  huduma pamoja na kupunguza mgao wa maji.
Hata hivyo amesema  wanakutana na changamoto nyingi wanapotoa huduma ikiwa ni pamoja na wizi wa maji,kupanda kwa madini aina ya fluoride,mahitaji ya maji kuongezeka kwa sababu ya idadi ya watu na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha ukosefu wa mvua. 

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru