CHAMA CHA WAALIMU CHAWAAGIZA WALIMU KURUDI MAKAZINI KUANZIA LEO.
Posted on
Aug 3, 2012
|
No Comments

Rais wa Chama Cha walimu Tanzania (CWT)Gratian Mukoba.
Chama cha walimu nchini Tanzania kimewaagiza wanachama wake kurudi kuanzia kazini kuanzia leo Agosti 3 mwaka 2012 kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Rais wa Chama hicho Gratian Mukoba amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mwisho wa mahakama Kuu Divisheni ya Kazi yaliyotolewa na Mh. Jaji Wambura kwenye shauri Na. 96 ya mwaka 2012.
Aidha amesema walimu wamerudi makazini wakiwa wamekata tama sana kutokana na hukumu ya mahakama.
