MMOJA AFA NA WENGINE KUJERUHUWA WAKATI POLISI IKITAWANYA MAANDAMANO YA CHADEMA MOROGORO
Posted on
Aug 27, 2012
|
No Comments

Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi Kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamani wa Chadema mjini hapa.
Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi.

Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya chadema