MSIBA MWINGINE WAIKUMBA FAMILIA YA RAMBO, SOMA HABARI ZAIDI HAPA...
Posted on
Aug 29, 2012
|
No Comments
Methali ya hakuna msiba usio na mwenzake imeendelea kuthibitika baada ya gwiji la filamu Marekani Sylvester Stallone al-maarufu ‘Rambo’ kufiwa na dada yake pekee kipenzi ikiwa ni wiki 6 tu zimepita tangu afiwe na mwanae Sage aliyekuwa na umri wa miaka 36 tu.
Dada wa Staa huyo anayetamba na filamu aliyoitengeneza ya ‘ The Expendables 1 & 2” aliyekuwa akiitwa Toni Ann Filit (48)amefariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa Saratani.
Filit amefariki katika nyumba ya mama yao Jackie Stallone iliyopo Santa Monica baada ya kuamua kurejea nyumbani humo kutoka hospitali ya UCLA.