RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA TAIFA LIVE LEO ALASIRI.
Posted on
Aug 1, 2012
|
No Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alasiri ya leo, Jumatano, Agosti Mosi, 2012, atazungumza na taifa kupitia Mkutano wa Waandishi wa Habari utakaofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Mkutano huo utakaoanza saa 10 kamili utahudhuriwa na Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi Watendaji, Wahariri Wakuu na Wahariri Watendaji na utatangazwa moja kwa moja na televisheni nchini.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Agosti, 2012