photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > SERIKALI KUAGIZA VICHWA VIPYA VYA TRENI 13 ILI KUONDOA ADHA YA USAFIRI WA RELI.

SERIKALI KUAGIZA VICHWA VIPYA VYA TRENI 13 ILI KUONDOA ADHA YA USAFIRI WA RELI.

Posted on Aug 28, 2012 | No Comments

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe

Serikali imesisitiza kuwa itaagiza vichwa vipya 13 vya treni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa huduma bora za Reli.
Hatua hiyo imetokana na kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa kukodi vichwa kutoka nje ya nchi ambavyo baadhi vimechakaa.
Vichwa hivyo vya kukodi vinakuwa ni mzigo mkubwa kwa serikali hali inayofanya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuviendesha huku baadhi vikiwa ni chakavu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishwaji wa mapendekezo ya  Kamati ya Ndogo ya Ushauri na Kutengeneza Sera za Reli, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe amesema vichwa vya kukodi vina gharama kubwa hivyo ni vyema vikaagizwa vipya.
Amesema Kamati ndogo ya Ushauri na kuitengeneza Sera ya Reli iliundwa ikiwa na majukumu mbalimbali, ambapo imekamilisha kazi yake na sasa inatoa mapendekezo ambayo yanatajadiliwa.
Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Dkt. Malima Bundara alisema Kamati yake imebaini changamoto nyingi ikiwemo ya udhaifu wa usafiri wa reli.
Amesema Miundombinu ya reli na uwekezaji wake imekuwa ni mbaya na kufanya usafiri kusuasua

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru