photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TAASISI TA MED INTERNATIONAL YA MAREKANI KUISAIDIA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR KUFIKIA KIWANGO KINACHOKUBALIKA KITEKNOLOJIA.

TAASISI TA MED INTERNATIONAL YA MAREKANI KUISAIDIA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR KUFIKIA KIWANGO KINACHOKUBALIKA KITEKNOLOJIA.

Posted on Aug 31, 2012 | No Comments

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi inayoshughulikia Taaluma ya Teknolojia ya Afya ya chuo Kikuu cha Brown Mjini Boston Nchini Marekani (Med Inaternationala ) Bw. Jayson Marwaha Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi mwenza wa Taasisi hiyo Bw. Han Shen Chia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia Ripoti ya Uchunguzi wa Afya uliofanywa katika Hospitali za Zanzibar iliyowasilishwa na Mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani Bw. Han Shen Chia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa Afya katika Hospitali za Zanzibar.
Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani Bw. Jayson Marwaha akielezea uchunguzi uliofanywa na Taasisi yake kwa kushirikiana na Watendaji wa Sekta ya Afya ya Zanzibar.
Taasisi inayoshughulikia Taaluma ya Teknolojia ya Afya ya chuo Kikuu cha Brown Mjini Boston Nchini Marekani (Med International) imelenga kuisaidia Zanzibar katika Sekta ya Afya ili kufikia kiwango kinachokubalika  Kiteknolojia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mwenza wa Taasisi hiyo Bw. Han Shen Chia wakati akikabidhi Ripoti ya utafiti wa Afya uliofanywa na Wataalamu wa Taasisi hiyo katika Hospitali za Unguja na Pemba.
Bw. Han Shen akiwa pamoja na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Med International  Bw. Jayson Marwaha amesema utafiti huo uliochukuwa takriban wiki 10 umejaribu kutoa hali halisi ya mapungufu na maeneo ambayo Taasisi yao inaweza kusaidia kitaaluma  na hata uwezeshaji.
Amesema Mipango inaendelea kuimarishwa ili kuona Taasisi hiyo inawatumia Wataalamu wa Sekta hiyo kuja kutoa mafunzo kwa Walimu wa Afya Zanzibar.
Bw. Han amefahamisha kwamba utaratibu wa kuwapata wataalamu hao hasa wakati wa kipindi cha joto ambacho wanakuwa mapumziko utazingatiwa zaidi.
Kwa upande wake Mwakilishi na Mkurugenzi wa Med International Bw. Jayson Marwaha amemueleza Balozi Seif kwamba utafiti wao kwa kuanzia utaangalia zaidi kuimarisha Hospitali za Mnazi Mmoja Unguja na ya Chake Chake Pemba.
Bw. Marwaha amesema mpango huo utafuatiwa pia na Taasisi za Nchi hiyo kuweka vitega uchumi vyao vya Sekta ya Afya hapo baadaye katika Visiwa vya Zanzibar.
Amefahamisha kwamba uwekezaji huo utazingatia na kutegemea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakavyoridhia mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti hiyo.
Akitoa shukrani zake kwa hatua za Uongozi wa Taasisi hiyo ya Med Inaternational katika kusaidia sekta ya Afya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema juhudi za Taasisi hiyo zimeanza kuonyesha mwanga wa matumaini katika sekta hiyo muhimu kwa Jamii.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru