photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > UVCCM MKOANI IRINGA WAPATA VIONGOZI WAPYA

UVCCM MKOANI IRINGA WAPATA VIONGOZI WAPYA

Posted on Aug 31, 2012 | No Comments

 
Rais Jakaya Kikwete Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa akihutubia katika moja ya mikutano ya chama hicho.

Jumuiya ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM, umefanya uchaguzi na kupata viongozi wapya watakaoongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mgombea ambaye amechaguliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti ni Bw. Kayugwa ambaye ameshinda kwa kupata kura 288 kati ya kura 463 halali zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana hao.
Nafasi nyinge ambazo zimeweza kupata viongozi wapya ni pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Bw. Deogius Kisega ambaye amepata kura 217, halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Bw. Mkenge amepita kwa kupata kura 165.
Aidha katika nafasi ya za baraza la wilaya kupitia wilaya ya Iringa vijijini Bi. Ratifa Mwasiposya amepita kwa kupata kura 392 akifuatiwa na Nuru Nkenge ambaye amepata kura 389 na Bi. Newton Mongi akiwa na kura 370.
Aidha wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa na baraza kuu la mkoa unawakilishwa na Bw. Alice Kibiki ambaye amepata kura, 233 akifuatiwa na Bw. Thomas Muyinga mwenye kura 162 kupitia wilaya ya Iringa vijijini.
Wajumbe wengine ambao wanawakilisha kwenye Baraza kuu la mkoa ni pamoja na Bw. Kanute Mhongole mwenye kura 243, akifuatiwa na Yuda Vakulule mwenye jumla ya kura 207,  na Thomas Myinga mwenye kura 199.
Viongozi hao wapya wa Jumuiya ya umoja wa vijana kupitia Chama cha Mapinduzi wamesema wanatarajia kuleta mapinduzi ya mabadiliko katika kuleta maendeleo ya vijana ikiwemo kuwawezesha vijana kujitegemea katika ajira.          

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru