photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WACHIMBA MIGODI AFRIKA KUSINI KUFUNGULIWA MASHTAKA

WACHIMBA MIGODI AFRIKA KUSINI KUFUNGULIWA MASHTAKA

Posted on Aug 30, 2012 | No Comments

Wachimba migodi wa Marikana waliokamatwa

Wendesha mashtaka wa serikali nchini Afrika Kusini wanasema kuwa wanajianda kuwafungulia mashtaka ya mauaji wachimba migodi wa mgodi wa Marikana.
Ripoti zinasema pia, wachimba migodi hao, wanakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo jaribio la mauaji ya wachimba migodi thelathini na wanne ambao waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Msemaji wa ofisi ya kiongozi wa mashtaka nchini humo, amesema ikiwa watu, ambao baadhi yao wamejihami wakiwakabili polisi na kutokee mauaji, wale watakaoshikwa na polisi watafunguliwa mashtaka ya mauaji, bila kujali wale waliofyatua risasi.
Polisi waliwapiga risasi wachimba migodi hao kufuatia ghasia na maandamano kuhusu mishahara.
Maafisa wawili wa polisi waliuawa kwenye machafuko hayo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru