photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WANAWAKE TOGO WAITISHA MGOMO WA NGONO MPAKA RAISI AJIUZULU.

WANAWAKE TOGO WAITISHA MGOMO WA NGONO MPAKA RAISI AJIUZULU.

Posted on Aug 27, 2012 | No Comments

Isabelle Ameganvi anasema mgomo huu unalengo wa kufikisha ujumbe wa kile wanachotaka.

Wanawake Togo wameitisha mgomo wa ngono kwa kipindi cha week nzima, kuanzia jumatatu mpaka pale rais wa nchi hiyo ajiuzulu.
Mgomo huu umehamasishwa na chama cha upinzani, kauli mbiu ya mgomo ni 'Let's Save Togo', kauli mbiu hii au mgomo huu unawaonganisha makundi 9 ya kijamii na vyama 7 vya upinzani Togo.
Kiongozi wa upinzani Isabelle Ameganvi anasema ngono inaweza kutumiwa kama slaa kwenye vita hivi na ikaleta mabadiliko kwenye siasa.
Mgomo huu unataka Raisi Faure Gnassingbe ambaye familia yake imeshikilia kiti hicho kwa zaidi ya miaka 40 sasa aachie ngazi.
"Tuna njia nyingi sana ya kuwaambia wanaume tunataka nini Togo" anasema Ameganvi, kiongozi wa kikundi cha wakinamama.
Anasema aliongozwa na migomo kama ile iliyotokea Liberia mwaka 2003 ambayo ililenga kuleta amani nchini humo.
"kama wanaume wakikataa kusikia tunachokitaka tutafanya mgomo wa kitu kingine kikubwa zaidi ya Ngono", Alisema.. Mfano kufunga kula.
Togo imeongozwa na familia mmoja kwa zaidi ya miaka 40 sasa...

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru