photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > HII NDIYO HOTUBA YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF KATIKA SIKU YA TIBA ASILI AFRIKA

HII NDIYO HOTUBA YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF KATIKA SIKU YA TIBA ASILI AFRIKA

Posted on Sep 2, 2012 | No Comments

HOTUBA YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA MAADHIMISHO YA KUMI YA SIKU YA TIBA ASILI - AFRIKA, HUKO BUSTANI YA VICTORIA MJINI ZANZIBAR TAREHE 31 AGOSTI, 2012 

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,
Waheshimiwa, wawakilishi wa mabalozi wadogo wa Jamhuri ya watu wa China na India.
Katibu Mkuu Wizara Afya, Waheshimiwa Waganga wa Tiba Asili,
Waalikwa nyote, mabibi na mabwana Asalaam Alaykum.

Kwanza kabisa sinabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukusanyika hapa kwa pamoja katika hafla ya kuadhimisha siku ya Tiba Asili Barani Afrika.

Vile vile, shukurani zangu za dhati kabisa nazielekeza kwenu waandaaji wa shughuli hii muhimu kwa ustawi na maendeleo ya afya za watu wetu, hao siwengine bali ni Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na wadau mbali mbali wa Tiba Asilia, kwa maandalizi yenu mazuri.

Na zaidi kwa uamuzi wenu wa kunialika mimi kuja hapa kujumuika nanyi katika hafla hii. Nasema ahsanteni sana.

Waheshimiwa viongozi, wataalamu na waalikwa wenzangu Siku ya leo tupo hapa kwa lengo maalum ambalo ni kusherehekea siku ya Tiba Asili – Barani mwetu Afrika, katika sherehe ambazo mwaka huu zimepewa kauli mbiu iliyo katika mfumo wa swali linalouliza
 “SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA KUMI YA TIBA ASILI BARANI AFRIKA, TUNAJIFUNZA NINI?

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru