HUYU NDIYE REDDS MISS KANDA YA MASHARIKI 2012
Posted on
Sep 2, 2012
|
No Comments
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas akiwa ni mwenye furaha baada ya kutajwa kuwa mshindi na kujinyakulia taji hilo baada ya kuwashinda warembo wengine 11 katika kinyanganyiro hicho cha aina yake.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Washiriki wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutajwa kufanikiwa kupita katikia hatua hiyo.
Kutoka kushoto ni 6. Zuhura Gora,
7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce Baluhi.
Warembo wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show kali ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo.