photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MAKAMU WA RAIS DK. BILAL NA WAKUU WA POLISI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA SARPCCO KUUNGANISHA NGUVU DHIDI YA UGAIDI

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL NA WAKUU WA POLISI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA SARPCCO KUUNGANISHA NGUVU DHIDI YA UGAIDI

Posted on Sep 5, 2012 | No Comments


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal amewataka Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika  (SARPCCO) kuunganisha nguvu zao kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zinakuwa salama muda wote, kutokana na vitisho vinavyoikabili Dunia.
 Amesema vitisho kama Ugaidi,Madawa ya kulevya,Uharamia na Usafirishaji wa watu ni matukio ya kihalifu ambayo yanafanywa kwa mitandao mirefu ya kimataifa hivyo Wakuu hao wanapaswa kuandaa mikakati ya pamoja kuweza kupambana na Vitisho hivyo.
 Dk.Bilali ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua Mkutano huo wa SARPCCO wenye lengo la kupanga mikakati ya kukabiliana na uhalifu kwa nchi wanachama uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Karume katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
 Amesema hakuna Nchi Duniani ambayo inaweza kutangaza kuwa iko salama kutokana na vitisho ikiwemo suala la Ugaidi lakini kama Jeshi la Polisi litakuwa makini muda wote hali ya vitisho inaweza kupungua.
 Amewataka Wakuu hao kufanya kazi kama Taifa moja ili kuzuia mianya yote ya kihalifu inayoweza kudhuru hali ya Usalama wa Jumuiya hiyo.
 Awali katika Hotuba yake Dk. Bilal amemuhakikishia Ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema ili kuiendesha Jumuiya hiyo kwa Ufanisi.
 Kwa upande wake Mwenyekiti huyo mpya wa SARPCCO IGP Mwema ametoa shukrani zake kwa kuaminiwa kuiendesha Jumuiya hiyo na kuahidi mafanikio makubwa kwa Nchi wanachama wa Jumuiya katika kipindi chote cha ungozi wake.
 Aidha IGP Mwema ameelezea mafanikio ya Jumuiya hiyo kuwa ni pamoja na kupunguza vitisho vya Uharamia na uhalifu mwengine wa Kimataifa katika nchi wanachama nakwamba hata mafanikio ya kuwakamata Wahalifu wa Madawa ya kulevya nchini Tanzania yanatokana na ushirikiano wakiintelijensia kutoka nchi wanachama.
 Akitoa hotuba yake Mwenyekiti Mstaafu wa SARPCCO ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini Mangwashi Victoria Phiyenga ameishukuru Serikali ya Muungano wa Tanzania kwa maandalizi mazuri ya Mkutano huo na kuahidi kumpa mashirikiano ya kutosha Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo.
 Mkutano huo wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika  (SARPCCO) ambao unafanyika Zanzibar una lengo la kupanga mikakati ya kukabiliana na uhalifu katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru