SIMBA YAINYUKA AFRICA LYON MAGOLI 3-0 KWENYE UWANJA WA TAIFA
Posted on
Sep 16, 2012
|
No Comments

Kwa matokeo ya leo ina maana kwamba timu ya Simba inaaza ligi hiyo ikiwa na pointi tatu na magoli matatu ukiwa ni mtaji tosha kwa kuanza, wakati huohuo mahasimu wao wakubwa timu ya Yanga ya Jangwani kutoka jijini Dar es salaam ilikuwa na kibarua kigumu kule mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine , wakati ilipokutana na timu iliyopanda daraja ya maafande wa Magereza “Prison”, katika mchezo huo matokeo yamekuwa 0-0 baada ya maafande hao kukaza buti na kuwazuia wana Yanga kwenye uwanja wa nyumbani kwao